Tuesday, February 16, 2021

#UJASILIAMALI: NAMNA YAKUTENGENEZA UBUYU WA ZANZIBARI

 MAHITAJI YA UBUYU WA ZANZIBAR

1.Sukari vikombe 2
2.Maji vikombe 2
3.Nusu kikombe unga wa ubuyu
4.Vikombe 4 ubuyu wenyewe
5.1/4 pili pili ya unga
6.1/4 tsp chumvi
7.1/4 tsp iliki ya unga
8.Rangi nyekundu au yeyote ile utakavyopenda.
9.vanilla(kama utapenda)
MATAYARISHO YA UBUYU WA ZANZIBAR
1.Katika sufuria,weka maji na sukari na chumvi na pili pili ya unga na Rangi na iliki. Moto uwe juu kiasi na changanya vyote hivyo vipike vizuri.
2.Wakati vitu vinaanza kujipika utakuta rojo linatoa mapovu. Endelea tu kukoroga acha rojo lipikike vizuri. Baada ya hapo mapovu yakianza kutulia inamaanisha kua rojo limeanza kua zito.
3.Sasa hapo chota kidogo katika mwiko na test kwa vidole kama rojo linanata ua halinati. Rojo linatakiwa linate ndio linakua limeiva. Lisinate Sana kiasi tu.
4.baada ya mchanganyiko wako kuiva ipua hayo maji sasa Chukua beseni au sufuria chini weka ubuyu wako ndani ya beseni Anza kumimina hiyo juice yako kidogo kidogo huku ukiuchanganya kwa mikono safi.Ila hakikisha pembeni una Unga wa ubuyu ulio changanywa na mchanganyiko huo huo.
5.Baada ya ubuyu wako kuchanganyika vizuri (usiwe rojo) Anza kumiminia ule unga kwa juu ili uwe mkavu mkavu na kutoa ule ubichi alafu uanike ukishapoa ubuyu tayari kuliwa.
NOTE:UNGA WA UBUYU MKAVU LAZIMA UCHANGANYIE NAO PIA PILI PILI,ILIKI NA RANGI
ANGALIZO:Hatua ya 4 ni muhimu sana hakikisha mchanganyiko unamimina kwenye ubuyu mkavu na sio kuchukua ubuyu mkavu na kuupikia.Tunafanya hivyo ilikufanya ubuyu uwe mlaini na usiwe mgumu wakati wakula.
USIPO ZINGATIA STEPS NILIZO KUPA BASI JIANDAE KUTOA UBUYU ROJO KILA UKIANDAA.


#UJASILIAMALI: TIPS/DONDOO ZA KEKI ILI IWE VIZURI.

 1.Kuoka ni sayansi hivyo ni muhimu Sana kuzingatia vipimo,hakikisha unapima kwa usahihi kila hitaji lako usiongeze wala kupunguza hitaji muhimu hasa unapojaribu kwa Mara ya kwanza.

2.Hakikisha umepima kila kitu mezani kabla ya kuanza upishi wa keki,zoezi la keki ni la haraka ili kuepusha keki kuanza kuumuka kabla ya kuingia katika oven na hatimaye kupata matokeo mabaya.Pia hakikisha oven umewasha tayari inapata moto.
3.Pendelea zaidi kuchekecha unga wako ili upate keki nyepesi na ya kuchambuka vizuri.
4.Paka chombo chako mafuta kisha nyunyiza unga ili kurahisisha keki kutoka kwa urahisi bila kushika kwa pan au zungusha kwa karatasi ya kuokea
5.Pendelea zaidi kutumia mwiko au spatula wakati wa kutia unga ili kuepusha kupiga Sana na kuua nguvu ya baking powder,NA kama utatumia machine basi changanya kwa speed ndogo kabisa.
6.Usifungue oven yako kabla ya nusu saa ya uokaji,ikiingia hewa wakati keki bado mbichi itanywea na kutoiva vizuri.Angalia maendeleo ya keki yako kupitia kioo cha oven yako. Kufungua fungua oven kunathiri pia moto na kuharibu keki yako.
7.Acha keki ipoe katika chombo chake kwa muda wa dk 10 kisha itoe iache ipoe kabisa kabla ya kukata au kupamba.Usiache keki ipoe katika pan moja kwa moja itatengeneza unyevu na hatimaye kusumbua kutoka wakati wa kutoa.keki unazoweza kuacha zipo katika chombo chake ni zile sticky au keki za kunata zenye matunda,asali nk pia coffee cakes ambazo zinakatwa zikiwa katika chombo chake.
8.Itie keki katika freezer kwa muda wa dk 15 ikiwa wataka kuipamba itakurahisisha kupamba kwa urahisi bila kupata crumbs nyingi.
9.Zingatia moto usiwe mkali wala mdogo,moto ukiwa mkali keki itaiva kwa haraka na kupasuka pia itakuwa kavu haiwezi kuchambuka na moto ukiwa mdogo itanywea na kuiva kwa kunata ndani hivyo zingatia Sana moto.
10.Tumia chombo kinachoendana na kipimo cha keki yako usitumie chombo kikubwa Sana keki itaiva kwa kusambaa na kutopanda vizuri pia usitumie chombo kidogo itaiva kwa kujibana na matokeo yake.


#UJASILIAMALI: JINSI YA KUPIKA MKATE KUMIMINA / SININIA / MCHELE NYUMBANI

 MAHITAJI NA VIPIMO.

I. 1 kikombe cha mchele
ii. 1 kikombe cha nazi ya unga
iii. 1 kikombe cha sukari kupungua kidogo
iv. 1 kikombe cha maji au maziwa vuguvugu
v. 1 kijiko cha chai cha hamira
vi. iliki kiasi upendavyo
vii. ute wa yai moja
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA.
i. Osha na kuroweka mchele siku moja ndani ya maji ya baridi.
ii. Saga ndani ya blender, mchele, tui, maji au maziwa, iliki, na hamira mpaka mchanganyiko uwe lani kabisa.
iii. Mimina ndani ya bakuli na ufinike. Weka mahali penye joto ili mchanganyiko uumuke(ufure).
iv. Mchanganyiko ukifura, washa oven moto wa 350°. Mimina sukari pamoja na ule ute wa yai ndani ya mchanganyiko na uchanganye vizuri.
v. Ukiona mchanganyiko ni mzito sana, ongeza maziwa kidogo.
vi. Chukua sufuria umimine mafuta kidogo. Washa jiko na uweke sufuria ipate moto kiasi.
vii. Mimina ule mchanganyiko ndani ya sufuria uuwache kama dakika 5 hivi kiasi mkate uanze kushikana.
viii. Funika sufuria na uvumbike(bake) ndani ya oven kama dakika 35-40 hivi, au mpaka mkate uive na uwe rangi ya hudhurungi juu yake.
ix. Epua na uwache upoe kabisa kabla ya kukata. Ni bora kuula siku ya pili yake.


#UJASILIAMALI: JINSI YAKUTENGENEZA BISCUTI ZA MAYAI

 MAHITAJI NA VIPIMO.

i. Unga ( Ngano ) 3 Vikombe
ii. Sukari ya unga (icing sugar) 1 Kikombe
iii. Siagi 250 gm
iv. Mayai 3
v. Vanilla 2 Vijiko vya chai
vi. Baking powder 1 Kijiko cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA.
i. Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy).
ii. Tia mayai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini.
iii. Tia unga na baking powder changanya na mwiko.
iv. Tengeneza round upange kwenye tray.
v. Nyunyuzia sukari juu ya hizo round ulizotengeneza kabla huja choma.
vi. Pika (bake) katika oven moto wa 350°F kama muda wa dakika 15 hivi huku
vii. Hakikisha uwe unazitazama tazama.
Note : Kama utapenda unaweza kuweka nukta ya rangi nyekundu ukiwa hatua ya IV.


#UJASILIAMALI: JINSI YAKUPIKA BOGA LA NAZI

 MAHITAJI NA VIPIMO.

i. Boga - 1
ii. Tui La Nazi - 2 Vikombe
iii. Sukari - 1 kikombe
iv. Hiliki - 1/2 kijiko cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Unamenya maboga kiasi ukipendacho.
2. Unayakata kata vipande vidogo vidogo.
3. Unayachemsha mpaka yawive lakini humwagi maji wala yasije kuvurugika.
4. Maji yakishaanza kukauka unatia sukari kiasi ukipendacho na hiliki.
5. Kisha unamimina tui la nazi.
6. Unaiwacha ichemkie na kabla kukauka tui unaepuwa na tayari kuliwa.



#UJASILIAMALI: JINSI YA KUPIKA KEKI ZA MAZIWA

 MAHITAJI NA VIPIMO

i. Siagi - Kikombe 1
ii. Sukari - Kikombe 1
iii. Unga - Vikombe 2
iv. Maziwa - 1/2 (nusu) Kikombe
v. Mayai - 4
vi. Baking Powder - 1 Kijiko cha supu
vii. Arki rose - kidogo
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Washa oveni 350 - 400 Deg C liache lishike moto huku ukitayarisha mchanganyiko wa keki.
2. Changanya sukari na siagi mpaka ichanganyike.
3. Mimina mayai na maziwa uchanganye vizuri.
4. Mimina Baking Powder kwenye unga na uchanganye vitu vyote pamoja na arki rose.
5. Endelea kuchanganya vizuri mpaka uhakikishe vimechanganyika vizuri (unaweza kufanya bila ya mashine)
6. Chukua trey ambayo haitojaa ukiimimina, ipake siagi na umimine mchanganyiko wako. Treya isiwe nzito sana au nyepesi sana bali iwe wastani.
7. Ipike (Bake ) mpaka iwive.
8. Epua iache ipoe ndio ukate kate vipande.


#UJASILIAMALI: JINSI YAKUPIKA BOFLO

 MAHITAJI NA VIPIMO.

Kipimo cha mikate miwili
i. Unga mweupe - 6 vikombe (29 ounces takriban)
ii. Hamira - 2 vijiko vya chai
iii. Siagi (butter) - 2 Vijiko vya kulia
iv. Maji ya dafudafu (warm water) - 1 kikombe
v. Maziwa dafudafu (warm milk ) - 1 kikombe
vi. Sukari - 2 Vijiko vya kulia
vii. Chumvi - 1 kijiko cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA.
1. Weka katika bakuli la mashine (electrical bowl) hamira, maziwa, sukari chumvi na siagi iliyoyaushwa. Changanya vizuri kwa mwiko.
2. Tia unga pole pole huku umeasha mashine ikande, ukiongezea unga mpaka umalizike.
3. Pakaza siagi bakuli jengine kubwa kisha mimina mchanganyiko. Funika kwa kitambaa kilichokuwa kimeloa maji (damp cloth) au karatasi ya plastiki (plastic wrap). Uache unga uumuke mpaka uwe saizi ya mara mbili yake.
4. Utoe hewa unga na umimine juu ya baraza (flat surface). Gawa mchanganyiko sehemu mbili umimine katika treya ya loaf (loaf pan) size ya treya 9 x 5 inchies takriban. Acha uumuke tena kiasi nusu saa.
5. Washa oveni mapema kiasi 200 Degrees uchome (bake) kaisi nusu saa mpaka ugeuke rangi ya hudhurungi (golden brown).
6. Epua upoe ukiwa tayari
#SHARE na wenzako wajifunze


#UJASILIAMALI: JINSI YA KUTENGENEZA SIAGI YA KARANGA ( PEANUT BUTTER ) NYUMBANI.

 MAHITAJI NA VIPIMO

i. Karanga vikombe 2
ii. Asali au sukari kijiko 1 na nusu cha chakula
iii. Mafuta ya kupikia kijiko 1 na nusu cha chakula
iv. Chumvi ½ kijiko cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUTENGENEZA SIAGI YA KARANGA.
1.Kaanga karanga bila mafuta mpaka zikaangike vizuri yani maganda yaanze kutoka yenyewe
2.Ziache zipoe kisha toa maganda
3.Mimina karanga,chumvi na mafuta katika blender ama food processor...saga hadi iwe laini
4.Ongeza asali,chumvi ,sukari au asali na mafuta saga hadi iwe laini...
5.Hifadhi katika chupa yako kisha weka kwenye Friji
NB ; UKILA NA MKATE USISHANGAE KUSIKIA KITU KINAKUAMBIA UKANUNUE MKATE MWINGINE MZIMA 😋
#SHARE na wenzako wajifunze

.


#UJASILIAMALI: JINSI YA KUPIKA JAM YA NANASI NYUMBANI.

 MAHITAJI NA VIPIMO

♦Nanasi kata vipandevipande
♦sukari nyeupe au yakawaida vikombe 2
♦ndimu vijiko 4
♦maji kikombe 1
JINSI YA KUANDAA NA KUPIKA JAM YA NANASI
1.Chemsha nanasi hadi likiwa laini lipondeponde
2.Tia sukari ktk sufuria na maji ukoroge mpaka iyeyuke
3.Iweke jikoni ichemke mpaka uone inanatanata ktk vidole tahadhari isiungue
4.Tia nanasi lako na maji ya ndimu changanya ,iwache ichemke kwa moto mdogo mdogo mpaka iwe nzito kama jam zengine kisha epua ,tayari kwa matumizi waweza kula na mkate,banzi nk.ENJOY! Je umeipenda?
#SHARE na wenzako wajifunze.



#UJASILIAMALI: JINSI YA KUPIKA TOMATO SAUCE / PASTE NYUMBANI

MAHITAJI NA VIPIMO VUA TOMATO SOUCE.
1. Nyanya Kg 1.5 ( Kilo moja na nusu
2.Vitunguu Maji. Vitatu vilivyo menywa na kukatwa katwa vipande.
3. Mafuta ya Kupikia Vijiko Sita Vya Chakula.
4. Sukari Vijiko viwili vya chai.
5. Citric Acid.
6.Vinegar (siki) Vijiko viwili vya chai.
NAMNA YA UPIKAJI TOMATO SAUCE
1. Saga mchanganyiko wa malighafi zote zilizo tajwa hapo juu kwa pamoja kwa kutumia mashine ya blender mpaka uwe rojo rojo.
2. Tenga jiko la mkaa lenye moto wa wastani, kisha injika kikaangio kwenye moto halafu weka mafuta ya kupikia vijiko sita vya chakula.
3. Mafuta yakianza kuchemka , anza kumimina mchanganyiko wako huo ndani ya kikaango hicho huku ukiwa una koroga upande mmoja mpaka umalize kuchanganya. Tumia dakika 15 kufanya zoezi hili.
* Utakapo ona mchemsho wako umeanza kuwa uji uji, ipua na weka kwenye chombo safi tayari kwa matumizi.
#SHARE na wenzako wajifunze.

#UJASILIAMALI: JINSI YA KUPIKA CHAPATI LAINI SANA.

MAHITAJI NA VIPIMO.
i. Unga mweupe wa ngano vikombe 4
ii. Samli safi vijiko 3 vya kulia
iii. Chumvii kijiko 1 chai
iv. Maji vuguvugu (warm) vikombe 2
v. Samli ya kupikia chapati.
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA.
1. Mimina unga, samli na chumvi kwenye sinia au bakuli kubwa. Changanya pamoja.
2. Mimina maji kidogo kidogo huku unachanganya na ule mchanganyiko wa unga.
3. Mchanganyiko ukishashikana, kanda unga kwa mkono kiasi, kama dakika tano hivi.
4. Finika na uache mchanganyiko kwenye sinia kama dakika kumi hivi kwa kuufunika ili hewa isiingie.
5. Gawanya ule mchanganyiko kwa kufanya madonge kama kumi na nne au kumi na sita kwa chapati ndogo.
6. Mimina unga kidogo mahali ambapo utasukuma chapati.
7. Sukuma donge moja mpaka liwe duwara jembamba.
8. Paka samli kama kijiko kimoja cha kulia, ukihakikisha umepaka duwara lote.
9. Kunja lile duwara kama mfano wa kamba, huku unazungusha kama kamba ili iwe ndefu kidogo.
10. Zungusha ile kamba iwe mviringo. Funika na kitambaa kisafi cha jikoni ambacho kimajimaji kidogo.
11. Endelea namna hii mpaka umalize madonge yote.
12. Sukuma chapati iwe mviringo kama nchi 7 hivi
13. Pika chapati kwenye frying pan moto wa kiasi. Ikiiva upande mmoja na kuanza kufura, geuza upande wa pili. Tumia kitambaa kisafi cha jikoni kupress na kuzungusha zungusha ile chapati. Ikiiva upande wa pili, mimina kijiko kimoja cha kulia cha samli na ugeuze chapati tena, zungusha zungusha kisha mimina nusu kijiko cha kulia cha samli na ugeuze upande wa pili kidogo. Toa chapati uweke kwenye sahani. Ikunje kunje kidogo kisha uifingue vizuri.
14. Endelea namna hii huku unafuta frying pan na kitambaa kisafi au karatasi za jikoni (tissue) baada ya kila chapatti.
KIDOKEZO.
1. Unapomaliza kuzipika kila moja, zitandaze kwanza chapati katika sahani (au sinia) kubwa zipate kupoa ziwe kavu ili zisinyonyanye mafuta. Kisha tena ziweke katika sahani yako ya kawaida.
2. Ni nzuri kutolea na jam au asali
#Share na wenzako wajifunze. Asanteni


#UJASILIAMALI: JINSI YA KUPIKA PILAU LA KUKU SIMPLE NYUMBANI.

MAHITAJI NA VIPIMO
i. Mchele wa basmati - 3 vikombe
ii. Kuku - ½
iii. Viazi - 4
iv. Vitunguu - 2
v. Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 2 vijiko vya supu
vi. Binzari ya pilau nzima - 1 Kijiko cha chakula
vii. Binzari ya pilau - ½ kijiko cha chai
viii. Pilipili manga nzima - ½ kijiko cha cha
ix. Karafuu nzima - 8
x. Iliki nzima - 6
xi. Mdalasini nzima - 5 vijiti
xii. Pilipili mbichi iliyosagwa - 2
xiii. Chumvi - kiasi
xiv. Mafuta ya kupikia - ¼ kikombe
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA.
1. Osha mchele na roweka kwa muda kutegemea na aina ya mchele.
2. Kata kuku vipande upendavyo, safisha kisha mchemshe kwa chumvi, pilipili iliyosagwa, thomu na tangawizi.
3. Akiwiva kuku, mtoe weka kando, bakisha supu katika sufuria.
4. Katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangu ya hudhurungi.
5. Tia thomu na tangawizi na binzari zote kaanga kidogo
6. Kisha tia viazi kanga kidogo kisha tia kisha tia vipande vyako vya kuku na supu acha ichemke kidogo kisha tia maji ukisie kutokana na mchele unaotumia.
7. Mwisho tia mchele koroga uchanganye na vitu vyote acha ichemke kiasi kisha funika na punguza mo mpaka uive (huku ukiugeuzageuza)
8. Ukishakuwa tayari pakua kwenye sahani tayari kwa kula na salad na pilipili.
#SHARE na wenzako wajifunze.


#UJASILIAMALI: JINISI YA KUPIKA BAGIA ZA KUNDE NYUMBANI.

 MAHITAJI

1- Vikombe 2 kunde
2- Kitunguu 1 kikubwa
3- Pilipili kichaa 2 (nyekundu na kijani ukipenda)
4- Vijiko 3 vya chakula maji ya limao (ukipenda)
5- Kijiko 1 cha chai baking powder
6- Vijiko 1½ vya chai tangawizi
7- ¼ kikombe majani ya giligilani
8- Chumvi kwa kuonja
9- Mafuta ya kukaangia
*MAELEKEZO*
1- Osha na kuloweka kunde kwenye maji ya moto siyo chini ya masaa 8, au usiku mzima
2- Katakata kitunguu, pilipili, majani ya giligilani; twanga tangawizi. Weka pembeni
3- Chuja kunde maji
4- Weka kunde, maji ya limao na pilipili kwenye mashine ya kusagia chakula au blender ila isilainike sana.
5- Unaweza pia kutumia mashine ya mkono ukipenda au kutwanga kwenye kinu. (hakikisha mashine yako ina nguvu ya kutosha kusaga kunde)
6- Ikilainika, ongeza kitunguu na majani ya giligilani kwenye mchanganyiko, saga kwa sekunde kama 20.
7- Hakikisha vitunguu na majani ya giligilani hayasagiki kabisa.
8- Weka mchanganyiko kwenye bakuli kubwa.
9- Ongeza chumvi na bakingo powder, changanya vizuri
10- Chemsha mafuta kwenye kikaango katika moto wa wastani.
11- Yakichemka, tumia vijiko 2 au mikono kutengeneza umbo kama la yai au umbo la bagia
12- Weka kwenye mafuta. Kaanga mpaka ziwe na rangi ya kahawia
13- Toa bhajiya zilizoiva kwenye mafuta.
14- Hamishia kwenye sahani/bakuli iliyowekewa tissues, au tumia chujio la bati ili mafuta yachuje
15- Pakua za moto na inapendeza kula na chachandu ya machicha ya nazi na mtindi
#SHARE na wenzako wajifunze.

#ELIMU-BURE

 Kitu muhimu zaidi kwenye kujenga ujuzi utakaokupa matokeo ni muendelezo.

Na hii ndipo hatua ya NNE unatakiwa kuizingatia.
Kuna wakati hautaona tofauti sana katika unachofanya kwa sababu haujafikia hatua ya kutoa matokeo yanayoonekana, usiache.
Watu wengi sana, huwa wanakata tamaa wanapoona wamefanya kwa muda fulani na hakuna matokeo na hakuna anayewaambia chochote kile.
Kwa mujibu wa mwanasaikolojia, Heidi Grant Halvorson anasema kuwa, watu wanaokuzunguka huwa wanaona 10% ya mabadiliko makubwa ya ujuzi ambayo utakuwa unayafanya kwenye maisha yako.
Hivyo, hata kama hakuna anayekuambia kuwa kuna mabadiliko, wewe usikubali kabisa kuacha kufanya.
Dhamiria kuwa mwaka huu utaweka nguvu na mwendelezo bila kuchoka hadi pale utakapokuwa umeona matokeo unayoyatafuta.
Usiache kwa sababu watu hawakusifii, weka mkazo kwenye kile unachokitafuta.
Kuna siku itakulipa.
Kumbuka watu wengi pia ni wagumu sana kusifia, hivyo sio kwamba hawaoni ila hawataki kusifia.
Songa mbele.
Kujifunza zaidi kwa kina kuhusu Namna ya Kupata Matokeo Makubwa Ndani ya Mwaka Mmoja Nashauri usoma eBook MPYA ya Strategy 2021.
Kuipata kwa Punguzo la 50% LEO
Tuma Tsh 5,000 Tu!
M-PESA
0756 094 875 (Ipyana Mwangoka)
Kisha tuma uthibitisho wa Muamala Whatsapp 0756 094 875.
NDANI YA MASAA 24 Utapokea eBook yako.
See You At The Top
Joel NanaukA




#UJASILIAMALI: NAMNA YAKUTENGENEZA UBUYU WA ZANZIBARI

  MAHITAJI YA UBUYU WA ZANZIBAR 1.Sukari vikombe 2 2.Maji vikombe 2 3.Nusu kikombe unga wa ubuyu 4.Vikombe 4 ubuyu wenyewe 5.1/4 pili pili y...