Tuesday, February 16, 2021

#UJASILIAMALI: NAMNA YAKUTENGENEZA UBUYU WA ZANZIBARI

 MAHITAJI YA UBUYU WA ZANZIBAR

1.Sukari vikombe 2
2.Maji vikombe 2
3.Nusu kikombe unga wa ubuyu
4.Vikombe 4 ubuyu wenyewe
5.1/4 pili pili ya unga
6.1/4 tsp chumvi
7.1/4 tsp iliki ya unga
8.Rangi nyekundu au yeyote ile utakavyopenda.
9.vanilla(kama utapenda)
MATAYARISHO YA UBUYU WA ZANZIBAR
1.Katika sufuria,weka maji na sukari na chumvi na pili pili ya unga na Rangi na iliki. Moto uwe juu kiasi na changanya vyote hivyo vipike vizuri.
2.Wakati vitu vinaanza kujipika utakuta rojo linatoa mapovu. Endelea tu kukoroga acha rojo lipikike vizuri. Baada ya hapo mapovu yakianza kutulia inamaanisha kua rojo limeanza kua zito.
3.Sasa hapo chota kidogo katika mwiko na test kwa vidole kama rojo linanata ua halinati. Rojo linatakiwa linate ndio linakua limeiva. Lisinate Sana kiasi tu.
4.baada ya mchanganyiko wako kuiva ipua hayo maji sasa Chukua beseni au sufuria chini weka ubuyu wako ndani ya beseni Anza kumimina hiyo juice yako kidogo kidogo huku ukiuchanganya kwa mikono safi.Ila hakikisha pembeni una Unga wa ubuyu ulio changanywa na mchanganyiko huo huo.
5.Baada ya ubuyu wako kuchanganyika vizuri (usiwe rojo) Anza kumiminia ule unga kwa juu ili uwe mkavu mkavu na kutoa ule ubichi alafu uanike ukishapoa ubuyu tayari kuliwa.
NOTE:UNGA WA UBUYU MKAVU LAZIMA UCHANGANYIE NAO PIA PILI PILI,ILIKI NA RANGI
ANGALIZO:Hatua ya 4 ni muhimu sana hakikisha mchanganyiko unamimina kwenye ubuyu mkavu na sio kuchukua ubuyu mkavu na kuupikia.Tunafanya hivyo ilikufanya ubuyu uwe mlaini na usiwe mgumu wakati wakula.
USIPO ZINGATIA STEPS NILIZO KUPA BASI JIANDAE KUTOA UBUYU ROJO KILA UKIANDAA.


#UJASILIAMALI: TIPS/DONDOO ZA KEKI ILI IWE VIZURI.

 1.Kuoka ni sayansi hivyo ni muhimu Sana kuzingatia vipimo,hakikisha unapima kwa usahihi kila hitaji lako usiongeze wala kupunguza hitaji muhimu hasa unapojaribu kwa Mara ya kwanza.

2.Hakikisha umepima kila kitu mezani kabla ya kuanza upishi wa keki,zoezi la keki ni la haraka ili kuepusha keki kuanza kuumuka kabla ya kuingia katika oven na hatimaye kupata matokeo mabaya.Pia hakikisha oven umewasha tayari inapata moto.
3.Pendelea zaidi kuchekecha unga wako ili upate keki nyepesi na ya kuchambuka vizuri.
4.Paka chombo chako mafuta kisha nyunyiza unga ili kurahisisha keki kutoka kwa urahisi bila kushika kwa pan au zungusha kwa karatasi ya kuokea
5.Pendelea zaidi kutumia mwiko au spatula wakati wa kutia unga ili kuepusha kupiga Sana na kuua nguvu ya baking powder,NA kama utatumia machine basi changanya kwa speed ndogo kabisa.
6.Usifungue oven yako kabla ya nusu saa ya uokaji,ikiingia hewa wakati keki bado mbichi itanywea na kutoiva vizuri.Angalia maendeleo ya keki yako kupitia kioo cha oven yako. Kufungua fungua oven kunathiri pia moto na kuharibu keki yako.
7.Acha keki ipoe katika chombo chake kwa muda wa dk 10 kisha itoe iache ipoe kabisa kabla ya kukata au kupamba.Usiache keki ipoe katika pan moja kwa moja itatengeneza unyevu na hatimaye kusumbua kutoka wakati wa kutoa.keki unazoweza kuacha zipo katika chombo chake ni zile sticky au keki za kunata zenye matunda,asali nk pia coffee cakes ambazo zinakatwa zikiwa katika chombo chake.
8.Itie keki katika freezer kwa muda wa dk 15 ikiwa wataka kuipamba itakurahisisha kupamba kwa urahisi bila kupata crumbs nyingi.
9.Zingatia moto usiwe mkali wala mdogo,moto ukiwa mkali keki itaiva kwa haraka na kupasuka pia itakuwa kavu haiwezi kuchambuka na moto ukiwa mdogo itanywea na kuiva kwa kunata ndani hivyo zingatia Sana moto.
10.Tumia chombo kinachoendana na kipimo cha keki yako usitumie chombo kikubwa Sana keki itaiva kwa kusambaa na kutopanda vizuri pia usitumie chombo kidogo itaiva kwa kujibana na matokeo yake.


#UJASILIAMALI: JINSI YA KUPIKA MKATE KUMIMINA / SININIA / MCHELE NYUMBANI

 MAHITAJI NA VIPIMO.

I. 1 kikombe cha mchele
ii. 1 kikombe cha nazi ya unga
iii. 1 kikombe cha sukari kupungua kidogo
iv. 1 kikombe cha maji au maziwa vuguvugu
v. 1 kijiko cha chai cha hamira
vi. iliki kiasi upendavyo
vii. ute wa yai moja
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA.
i. Osha na kuroweka mchele siku moja ndani ya maji ya baridi.
ii. Saga ndani ya blender, mchele, tui, maji au maziwa, iliki, na hamira mpaka mchanganyiko uwe lani kabisa.
iii. Mimina ndani ya bakuli na ufinike. Weka mahali penye joto ili mchanganyiko uumuke(ufure).
iv. Mchanganyiko ukifura, washa oven moto wa 350°. Mimina sukari pamoja na ule ute wa yai ndani ya mchanganyiko na uchanganye vizuri.
v. Ukiona mchanganyiko ni mzito sana, ongeza maziwa kidogo.
vi. Chukua sufuria umimine mafuta kidogo. Washa jiko na uweke sufuria ipate moto kiasi.
vii. Mimina ule mchanganyiko ndani ya sufuria uuwache kama dakika 5 hivi kiasi mkate uanze kushikana.
viii. Funika sufuria na uvumbike(bake) ndani ya oven kama dakika 35-40 hivi, au mpaka mkate uive na uwe rangi ya hudhurungi juu yake.
ix. Epua na uwache upoe kabisa kabla ya kukata. Ni bora kuula siku ya pili yake.


#UJASILIAMALI: JINSI YAKUTENGENEZA BISCUTI ZA MAYAI

 MAHITAJI NA VIPIMO.

i. Unga ( Ngano ) 3 Vikombe
ii. Sukari ya unga (icing sugar) 1 Kikombe
iii. Siagi 250 gm
iv. Mayai 3
v. Vanilla 2 Vijiko vya chai
vi. Baking powder 1 Kijiko cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA.
i. Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy).
ii. Tia mayai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini.
iii. Tia unga na baking powder changanya na mwiko.
iv. Tengeneza round upange kwenye tray.
v. Nyunyuzia sukari juu ya hizo round ulizotengeneza kabla huja choma.
vi. Pika (bake) katika oven moto wa 350°F kama muda wa dakika 15 hivi huku
vii. Hakikisha uwe unazitazama tazama.
Note : Kama utapenda unaweza kuweka nukta ya rangi nyekundu ukiwa hatua ya IV.


#UJASILIAMALI: JINSI YAKUPIKA BOGA LA NAZI

 MAHITAJI NA VIPIMO.

i. Boga - 1
ii. Tui La Nazi - 2 Vikombe
iii. Sukari - 1 kikombe
iv. Hiliki - 1/2 kijiko cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Unamenya maboga kiasi ukipendacho.
2. Unayakata kata vipande vidogo vidogo.
3. Unayachemsha mpaka yawive lakini humwagi maji wala yasije kuvurugika.
4. Maji yakishaanza kukauka unatia sukari kiasi ukipendacho na hiliki.
5. Kisha unamimina tui la nazi.
6. Unaiwacha ichemkie na kabla kukauka tui unaepuwa na tayari kuliwa.



#UJASILIAMALI: JINSI YA KUPIKA KEKI ZA MAZIWA

 MAHITAJI NA VIPIMO

i. Siagi - Kikombe 1
ii. Sukari - Kikombe 1
iii. Unga - Vikombe 2
iv. Maziwa - 1/2 (nusu) Kikombe
v. Mayai - 4
vi. Baking Powder - 1 Kijiko cha supu
vii. Arki rose - kidogo
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Washa oveni 350 - 400 Deg C liache lishike moto huku ukitayarisha mchanganyiko wa keki.
2. Changanya sukari na siagi mpaka ichanganyike.
3. Mimina mayai na maziwa uchanganye vizuri.
4. Mimina Baking Powder kwenye unga na uchanganye vitu vyote pamoja na arki rose.
5. Endelea kuchanganya vizuri mpaka uhakikishe vimechanganyika vizuri (unaweza kufanya bila ya mashine)
6. Chukua trey ambayo haitojaa ukiimimina, ipake siagi na umimine mchanganyiko wako. Treya isiwe nzito sana au nyepesi sana bali iwe wastani.
7. Ipike (Bake ) mpaka iwive.
8. Epua iache ipoe ndio ukate kate vipande.


#UJASILIAMALI: JINSI YAKUPIKA BOFLO

 MAHITAJI NA VIPIMO.

Kipimo cha mikate miwili
i. Unga mweupe - 6 vikombe (29 ounces takriban)
ii. Hamira - 2 vijiko vya chai
iii. Siagi (butter) - 2 Vijiko vya kulia
iv. Maji ya dafudafu (warm water) - 1 kikombe
v. Maziwa dafudafu (warm milk ) - 1 kikombe
vi. Sukari - 2 Vijiko vya kulia
vii. Chumvi - 1 kijiko cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA.
1. Weka katika bakuli la mashine (electrical bowl) hamira, maziwa, sukari chumvi na siagi iliyoyaushwa. Changanya vizuri kwa mwiko.
2. Tia unga pole pole huku umeasha mashine ikande, ukiongezea unga mpaka umalizike.
3. Pakaza siagi bakuli jengine kubwa kisha mimina mchanganyiko. Funika kwa kitambaa kilichokuwa kimeloa maji (damp cloth) au karatasi ya plastiki (plastic wrap). Uache unga uumuke mpaka uwe saizi ya mara mbili yake.
4. Utoe hewa unga na umimine juu ya baraza (flat surface). Gawa mchanganyiko sehemu mbili umimine katika treya ya loaf (loaf pan) size ya treya 9 x 5 inchies takriban. Acha uumuke tena kiasi nusu saa.
5. Washa oveni mapema kiasi 200 Degrees uchome (bake) kaisi nusu saa mpaka ugeuke rangi ya hudhurungi (golden brown).
6. Epua upoe ukiwa tayari
#SHARE na wenzako wajifunze


#UJASILIAMALI: NAMNA YAKUTENGENEZA UBUYU WA ZANZIBARI

  MAHITAJI YA UBUYU WA ZANZIBAR 1.Sukari vikombe 2 2.Maji vikombe 2 3.Nusu kikombe unga wa ubuyu 4.Vikombe 4 ubuyu wenyewe 5.1/4 pili pili y...