Tuesday, February 16, 2021

#UJASILIAMALI: JINSI YAKUPIKA MAHARAGE YA MCHUZI WA NAZI


 Maharage - 3 Vikombe

1. Tui la nazi zito - 1½ kikombe
3. Kitunguu - 1 kikubwa
3. Nyanya - 2 au tatu
4. Kitunguu saumu (thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
5. Bizari ya mchuzi - 1 kijiko cha chai
6. Bizari ya manjano - robo kijiko
7. Pilipili mbichi - 3
8. Chumvi - Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
i. Roweka maharage, kisha chemsha maharage hadi yawive yabakie na supu yake kidogo
ii. Katakata kitunguu, nyanya, na thomu
iii. Kaanga kitunguu kidogo kisha tia thomu, nyanya, kisha kaanga,
iv. Tia bizari ya mchuzi na ya njano kaanga kidogo.
v. Tia tui la nazi na acha kidogo tu katika moto.
vi. Weka chumvi kiasi na koroga iliuonje, kisha tupia pilipili mbichi, mimina katika chombo yakiwa
tayari kuliwa


No comments:

Post a Comment

#UJASILIAMALI: NAMNA YAKUTENGENEZA UBUYU WA ZANZIBARI

  MAHITAJI YA UBUYU WA ZANZIBAR 1.Sukari vikombe 2 2.Maji vikombe 2 3.Nusu kikombe unga wa ubuyu 4.Vikombe 4 ubuyu wenyewe 5.1/4 pili pili y...